Ijumaa , 24th Sep , 2021

Game ya BongoFlava imechangamka sana kuanzia nusu ya mwaka huu 2021, kwani hatujazoea kuona wasanii wakubwa kama Alikiba Diamond na Harmonize kuachia ngoma zao kwa wakati mmoja.

Kutoka kushoto ni Alikiba, Harmonize na Rayvanny

Suala hilo limetokea mwaka huu baada ya Diamond Platnumz kuachia wimbo wa 'iyo' siku ya Julai 26, kisha siku nne baadaye Julai 30, Alikiba akaachia ngoma yake Jealous na Harmonize akaachia mang'dakiwe remix August 6.

Sasa vita hiyo wameihamishia kwa wasanii wanaowamiliki ambapo Alikiba ameachia kazi mpya aliyofanya na msanii wake Tommy Flavour inaitwa jah jah siku ya jana Septemba 23.

Kutoka Konde Gang Music, CEO Harmonize ametangaza ujio mpya ya msanii wake Cheed siku ya leo Septemba 24, kwa mara ya kwanza tangu aondoke lebo ya Kings Music Records.

Aidha msanii Rayvanny kutoka 'WCB' naye ametangaza ujio wa msanii wake Macvoice kwenye lebo yake mpya ya 'Next level music' siku ya Septemba 24.

Watoto wa mjini wanasema kimeumana, acha tuone wasanii hao kutoka lebo hizo watatoa ushindani kama kaka zao walivyofanya au la.