Binti aliyeolewa na Babu wa kizungu aibua mapya

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Unaambiwa umri ni namba tu kwenye mahusiano, kwani msanii Azzy Superstar amesema haoni noma kuwa kwenye mapenzi na mume wake wa kizungu Mr Wolfgang kutoka nchini Austria ambaye amempita miaka 32.

Azzy Superstar na mume wake Mr Wolfgang

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Azzy Superstar amesema ameshakuwa kwenye mahusiano na vijana wenzie lakini wakaamuumiza hivyo bora alelewe mzungu huyo ili oane raha.

"Watu wanaponda mahusiano wanasema nafata pesa kwa mume wangu kitu ambacho sio kweli kwa sababu nimesha-date na wanaume ambao wapo na uwezo chini yangu wakasema nawalea, kwa hiyo acha na mimi nilelewe nione raha maana nishalea sana na mimi nimechoka" amesema Azzy Superstar 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video