Alhamisi , 26th Nov , 2015

Star wa muziki kutoka Nigeria Damini Ogulu, aka Burna Boy anajipanga kumaliza kifungo chake cha kuingia nchi za Ulaya kwa namna ya aina yake, akiwa tayari katika mpango wa kufanya onesho lake mwaka kesho, tukio ambalo binafsi amelipania sana.

Staa wa muziki kutoka Nigeria Damini Ogulu, aka Burna Boy

Hii itakuwa ni nafasi ya star huyo kuingia katika nchi hizo za umoja wa Ulaya baada ya kipindi cha miaka 5 kupita, jaribio lake la kwanza kuingia nchini humo wakati bado akiwa na zuio likipelekea kukamatwa katika uwanja wa ndege na kurudishwa mara moja kwao Nigeria.

Star huyo alifungiwa kuingia UK baada ya kuhusishwa na tukio la mauaji, ambapo alihukumiwa na baadaye kuachiwa, na kuamua kurejea Nigeria kuendeleza shughuli zake nyingine ikiwepo muziki.