Jumanne , 28th Oct , 2014

Rapa Chidi Benz, amefikishwa katika mahakama ya Kisutu leo na kusomewa mashtaka yake kutokana na kosa la kupatikana na Dawa za Kulevya aina ya Heroine mwishoni mwa wiki iliyopita.

Chidi Beenz akiwa chini ya ulinzi mahakamani leo

Kutoka katika tukio hilo, Chidi amepatikana na makosa matatu ikiwepo kukutwa na dawa hizo haramu, kusafirisha dawa na pia kukutwa na vifaa vya kutayarisha uvutaji, utumiaji wa dawa hizo za kulevya.

Msanii huyu ametakiwa kurudi rumande mpaka tarehe 11 mwezi Novemba ambapo kesi itatajwa tena, huku dhamana yake ikiwekwa wazi kwa masharti wa kuwa na wadhamini wawili wakuaminika pamoja na shilingi milioni 1.