Alhamisi , 14th Mei , 2015

Mwigizaji maarufu wa kimataifa mwenye asili ya Zimbabwe, Danai Gurira anatarajiwa kushiriki katika project nyingine kubwa ya filamu huko Hollywood, 'The Legend of the Stolen Guitar' ambayo ipo katika hatua za awali za utayarishaji.

muigizaji nyota wa Marekani mwenye asili ya Zimbabwe Danai Gurira

Danai atashiriki sambamba na msanii mwingine maarufu wa muziki kutoka Zimbabwe, Thomas "Mukanya" Mapfumo, kazi hii nzima ikiwa chini ya mtayarishaji Austin Handriade ambaye pia asili yake ni Zimbabwe.

Danai ambaye amejijengea jina kubwa kutoka katika ushiriki wake katika filamu ya muendelezo ya Walking Dead, akiwa anatumia jina Michonne, anatarajiwa kuongeza chachu katika kisa cha filamu hiyo ambayo itaanza kuonekana rasmi mwaka 2016.