Alhamisi , 14th Jan , 2016

Star wa maigizo wa kimataifa wa huko Marekani ambaye asili yake ni Zimbabwe, Danai Gurira anatarajiwa kushiriki katika filamu mpya ya maisha ya nyota wa muziki wa Hip Hop, Hayati Tupac Shakur ambayo itasimama kwa jina 'All Eyes On me'.

Staa wa maigizo wa Marekani ambaye asili yake ni Zimbabwe, Danai Gurira

Danai atavaa uhusika wa mama wa 2 Pac, Afeni Shakur akitarajiwa kuungana na mwigizaji Demetrius Shipp JR ambaye ndio atavaa uhusika wa marehemu 2Pac katika kazi hiyo.

Danai amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujijengea umaarufu kupitia ushiriki wake katika filamu ya muendelezo ya Walking Dead, akishiriki ndani yake kama Michonne, akitarajiwa kuonesha uwezo zaidi ya huo katika project hiyo kubwa.