Jumatatu , 5th Sep , 2016

Nyota wa muziki na filamu, Ummy Wenceslaus maarufu kama ‘Dokii’ amesema ameridhishwa sana na jinsi ambavyo shindano la Dance100% linaibua vipaji vya wasanii wa kucheza nchini na kuongeza kuwa kwa kiwango chao wanafaa kushiriki shughuli za kitaifa

Kundi la J. Combat

Dokii ameyasema hayo aliposhiriki kutazama hatua ya nusu fainali ya shindano la Dance100% iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya nchini.

“Ukweli mimi ni mara yangu ya kwanza kutizama shindano hili ila nimegundua kumbe kuna burudani ya aina yake, kuna makundi mawili yamenifanya niamini kwamba kuna vipaji vingi sana ambavyo havijukani nchini na kiwango cha washiriki wanafaa kushiriki shughuli za kitaifa za kijamii na kiserikali katika kuburudisha umma” Amesema Dokii.

Dokii ameweka bayana kuwa pamoja na kwamba makundi 10 yameshiriki hatua ya nusu fainali ila makundi mawili yameonesha ustadi wa hali ya juu, na kutaja makundi hayo kuwa ni J Combati pamoja na Team Makorokocho.

Matukio yote ya Dance100% yanapatikana kupitia website ya www.eatv.tv/dance100 na kuoneshwa na EATV kila Jumapili saa moja jioni.

Msanii nyota wa muziki na filamu, Ummy Wenceslaus maarufu kama ‘Dokii’
Tags: