Alhamisi , 20th Nov , 2014

Msanii wa muziki Diamond Platnumz, siku ya leo ameachia rasmi zawadi nyingine kwa mashabiki wake, Ngoma Mpya pamoja na Video ya kazi inayosimama kwa jina 'Ntampata Wapi'.

msanii wa bongofleva Diamond Platnumz

Video hii ni kazi nyingine ya kuvutia na ya kiwango cha hali ya juu kutoka kwa muongozaji wa video wa Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Godfather, kazi ambayo imetambulishwa kwa mara ya kwanza hapa EATV.