Jumamosi , 14th Feb , 2015

Star wa muziki Gosby amefafanua kitendo chake cha kuamua kumuimba mpenzi wake ambaye pia ni star wa muziki Cindy Rulz katika ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Noma,

Cindy Rulz na Gosby

Amesema kuwa watu wengi huogopa kuweka mahusiano yao wazi kutokana na kuogopa usumbufu na maneno mengi kutoka kwa watu na mashabiki.

Gosby amesema kuwa, kila wapenzi wanakuwa na makubaliano ya namna ya kuendesha mahusiano yao, kwa upande wake na Cindy wakiwa na utaratibu wa kujiachia tangu siku ya kwanza na hapa anaeleza zaidi juu ya hili mwenyewe. NOMA.