Jumanne , 20th Oct , 2015

Homa ya ujio wa star wa kimataifa Wizkid kutoka Nigeria ambaye atatumbuiza jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club tarehe 31 mwezi huu ikiwa ni siku chache tu kupita baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, inazidi kupanda.

msanii nyota wa Nigeria Wizkid anayetarajia kutua Bongo kwa ajili ya onyesho kubwa la muziki

Tayari viiingilio vya onesho hilo vimekwishawekwa wazi ambapo utapata burudani yote kwa kingilio cha shilingi 20,000 tu kwa tiketi ya kawaida na shilingi 100,000 kwa VIP, mzigo mzima utaanza saa 12 jioni pale Leaders Club.

Endelea kutufuatilia kwa karibu kufahamu juu ya wasanii ambao watamsindikiza staa huyo kwa kimataifa jukwaani na vile onesho zima litakavyosukwa kuhakikisha unapata burudani iliyokidhi viwango.