Ijumaa , 25th Dec , 2015

Rapa 50 Cent amemshtaki Rick Ross kwa madai ya kuchukua sehemu ya wimbo wake wa 'In Da Club' na kuuchanganya kwenye albamu yake mpya ya 'Black Market'.

Rick Ross na Rapa 50 Cent

50 Cent, ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, amedai kuwa Ross amevunja sheria kwa kutumia wimbo wake kujitangaza bila ya ruhusa yake.

Ross amerap 'In Da Club' katika michano huru ya mixtape ya 'Renzel Remixes,' ambayo anaitumia kuitangaza albamu yake mpya. 50 Cent sasa anadai dola milioni 2 kama fidia.