Jumatatu , 15th Dec , 2014

Msanii mahiri wa filamu hapa Bongo, Jacquie Pentenzel amesema kuwa, kikwazo kikubwa kinachokwamisha makundi mengi hasa ya wasanii hapa Bongo ni kutanguliza uchu wa madaraka na maslahi mbele.

muigizaji wa filamu nchini jacqueline Pentenzel

Msanii huyu amesema kuwa, tatizo hili linaathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo na ukuaji wa sekta hiyo, ingawa sasa wasanii wameamua kufunguka na kuunda umoja huo katika ngazi ya kimataifa zaidi.