Kauli ya Chidi Benz kuhusu matukio ya kiki

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Msanii wa HipHop Chidi Benz amesema anashangaa kuona watu wanaohoji kuhusu matukio ya kiki kwa sababu ulimwengu mzima ndiyo unaelekea huko kutokana na uwepo na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Msanii wa HipHop Chidi Benz ndani ya studio za East Africa Radio

Akizungumzia hilo kwenye show ya Planet Bong ya East Africa Radio Chidi Benz amesema 

"Sijaelewa kwanini watu hawataki kiki na wanajua kabisa tupo wakati wa kiki, twende mbele turudi nyuma Ulimwengu wa sasa ni kiki, mitandao haiwezi kuwa mingi halafu kusiwe na kiki, inapoteza kwa sababu watu wengine wanaangalia zaidi kuliko kazi"

"Watu wasilazimishe kusema kiki inaua au inazingua, kama unasema inazingua achana na mitandao kama Facebook, Instagram na Twitter maana ndiyo inafanya mitandao inauza kwa kupata likes nyingi na views wengi,  wanakosea wanaposema kiki ni mbaya" Chidi Benz