Kisa Fredy Sponsa amuachia Nai kwa Moni yake

Jumamosi , 21st Nov , 2020

Sponsa amuachia Nai kwa Moni yake ni 'comment' ambayo ameiandika shabiki baada ya msanii Moni Centrozone kushea 'cover' ya wimbo mpya wa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Official Nai.

Picha ya pamoja ya Official Nai na Mone Centrozone

Kuvunjika kwa penzi lao kumefanya kuzungumziwa sana mitandaoni siku za hivi karibuni, pia wamekuwa wakirushiana maneno kwenye mistari ya nyimbo zao na 'interview' wanazozifanya.

Sasa kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV Official Nai amefunguka kila kitu kuhusu chanzo cha kuachana kwao ambapo amesema Moni alimuhisi anatoka na mfanyabiashara Fredy.

"Haya yanayoendelea mtandaoni yalianza nilipokwenda kwa Fredy kuongea naye biashara, comment zikawa nyingi lakini mimi sina mahusiano naye mwanzoni hata yeye alidhani mimi nafanya kiki lakini si kweli, tulipoanza ugomvi mimi niliondoka kwa Moni nikawa nakaa peke yangu tukawa tunawasiliana lakini baadaye ikafikia hatau kila mtu na mambo yake" amesema Official Nai

Kwa sasa Official Nai ameingia rasmi kwenye biashara ya muziki na ametoa wimbo wake mpya wa 'sisi sio saizi yao' ambapo mwanzo alikuwa video vixen.