Jumatano , 26th Nov , 2014

Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Staa wa Filamu na Muziki hapa Bongo, marehemu Sharomillionea, msanii aliyefanya kazi kwa karibu na Marehemu, Kitale amejipanga kwa ajili ya kuachia filamu ya mwisho aliyofanya naye.

muigizaji wa filamu Kitale akiwa na marehemu Sharomillionea

Filamu hiyo ambayo ni maalu ya kumuenzi sharo inakwenda kwa jina Safara Hasara na kwa mujibu wa Kitale, itawagusa wengi kutokana na matukio ndani yake, ikiwa pia na baadhi ya scene ambazo zilifanyika huko Tanga kipindi kifupi kabla ya tukio la ajali iliyochukua maisha yake.

Marehemu Sharomillionea alifariki dunia miaka 2 iliyopita tarehe kama ya leo katika Kijiji cha Lusanga huko Muheza Tanga akiwa safarini kuelekea nyumbani kwao.