Alhamisi , 16th Nov , 2017

Msanii Afande Sele amesema kitendo cha watu kumwambia kuwa anafanya vibaya kumsema marehemu (Steven Kanumba) ni kitendo ambacho kimepitwa na wakati na mila zisizofaa.

Afande Sele ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, huku akimjibu Mrisho Mpoto baada ya kumwambia anakosea kumsema marehemu kuwa alikuwa anabaka, na kusema kwamba mila kama hizo hazifai kwenye jamii kwani zinaleta madhara makubwa baadaye.

Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba ni ukweli usiopingika kuwa Kanumba alikuwa anafanya dhambi, hivyo ni jambo ambalo halitakiwi kufichwa ili wengine wajifunze kupitia hilo.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa baada ya muigizaji ELizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa kwa kifo cha Kanumba, na baadhi ya watu kusema kuwa alistahili adhabu hiyo huku wenine wakidai ameonewa kwani marehemu alikuwa anamrubuni kutokana na kuwa na umri mdogo kwake.

Msikilize Afande Sele hapa chini