Jumanne , 20th Jan , 2015

Muigizaji nyota wa filamu ambaye pia ni muongozaji mahiri wa filamu aliyetwaa tuzo ya Oscar Lupita Nyong'o anatatrajia kutua nchini Uganda mwezi Machi kuigiza katika filamu mpya iliyobatizwa jina Queen of Katwe.

Muigizaji nyota wa nchini Kenya Lupita Nyong'o

Filamu hiyo ambayo inahusu simulizi ya ukweli kuhusu mchezaji nyota wa kike wa mchezo wa drafti Phiona Mutesi, aliyetokea katika maisha duni hadi kufikia hatua ya ushiriki wake katika mashindano makubwa ya mchezo huo.

Katika uhusika wa filamu hiyo ya Queen of Katwe itakayopigwa picha nchini Uganda na Afrika Kusini, Lupita ataigiza kama mama yake mdogo na Phiona aitwaye Harriet Mutesi.