Jumatano , 10th Dec , 2014

Mwigizaji wa kimataifa mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong'o, ameendelea kutumia nafasi na mafanikio yake nje ya tasnia ya filamu kutoa hamasa kwa jamii inayomzunguka kufahamu kuwa mafanikio ya ndoto za kila mtu yanawezekana.

muigizaji nyota wa nchini Kenya Lupita Nyong'o

Mwigizaji huyu amepata nafasi ya kuzungumza katika mkutano wa wanawake uliokuwa na waudhuriaji wapatao 10,000 huko Massachusetts ambapo ametumia nafasi hii kueleza namna alivyopitia changamoto mbalimbali ikiwepo hofu ya kuchukua hatua kuelekea ndoto yake ya uigizaji.

Mwigizaji huyu staa ameweka wazi kuwa, yeye binafsi kama ilivyo kwa watu wengi alifikia kipindi alikuwa amechanganyikiwa kwa kutokufahamu anataka kuwa nani, kitu kilichomsumbua kwa muda mpaka pale alipochukua hatua ya kwanza kwenda kusoma masuala ya filamu.