Jumatatu , 26th Jul , 2021

Meneja Maneno amenyoosha maelezo kuhusu stori zinazosemekana kwamba huwa anawapeleka wasanii wake kwa waganga ili waweze ku-hit kwenye muziki kwa kusema watu wanaomsema hivyo wanamkosea na haamini kwenye ushirikina.

Meneja Maneno

"Wananikosea sana mimi namuamini Mungu, isipokuwa kwenye kutafuta maisha kuna njia nyingi kwahiyo inategemea na imani ya mtu lakini siamini kwenye ushirikina kwamba ukifanya hivyo ndio umefanikiwa kwa sababu kuna wasanii wengi wanafanya vizuri na hawajapitia huko" amesema Meneja Maneno 

Meneje Maneno tayari ameshafanya kazi ya kuwasimamia wasanii wakubwa Bongo kama TID, Hemedy PHD, Rich Mavoko, Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na sasa yupo na Sholo Mwamba.