Jumamosi , 26th Sep , 2015

Mtayarishaji muziki Mona Gangster kutoka studio ya Classic Sound, amesema kuwa sasa ni wakati ambapo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka na rahisi kurekebisha mfumo wa sasa katika soko la muziki unaotoa mwanya kwa wanyonyaji kufaidika.

Mona Gangster

Mona Gangster amesema hayo akilinganisha namna ambavyo kumekuwa na wepesi wa kushughulikia wasanii pale ambapo wanaonekana kuwa wamekosea ama kukiuka maadili, huku kukiwa na uwezekano wa kuchukua hatua kadhaa kuondosha ama kuziba mianya inayotumiwa na wanyonyaji wa kazi za sanaa.

Kuhusiana na hilo, Mona Gangster anaeleza zaidi hapa mwenyewe.