Jumatatu , 9th Mar , 2015

Staa wa filamu Yvonne Cherryl, maarufu zaidi kama Monalisa akiwa na miaka mingi katika tasnia hiyo bila kuwa na rekodi ya skendo, ametoa angalizo kwa wasanii hususan wale wanaochipukia katika fani hiyo.

muigizaji wa filamu Tanzania Yvonne Cherryl aka Monalisa

Muigizaji huyo mahiri amewasisitiza chipukizi hao kuweka nguvu na akili zaidi katika vipaji vyao, ikiwa ndio njia pekee ya kufanikiwa katika fani hiyo.

Monalisa ambaye ameonyesha kuwa na malengo mazito kisiasa pengine hapo baadae, amewataka wasanii wale wanaofikiria skendo ndio njia ya kujiongezea umaarufu, kufikiria kesho yao, na kama heshima wanazojivunjia sasa zitatoa nafasi kwa wao kupata nafasi katika uongozi hapo baadae.