Jumatano , 19th Aug , 2015

Kundi nyota la muziki wa miondoko ya reggae kutoka Jamaica Morgan Heritage wanatarajia kuwasili mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu nchini Kenya kwa ajili ya kufanya onesho kubwa la muziki ikiwa ni moja ya ziara yao kubwa duniani.

kundi nyota la muziki wa miondoko ya reggae kutoka Jamaica Morgan Heritage

Morgan Heritage wameelezea kuwa baada ya kuweza kutumbuiza nchini Kenya mwaka 2009, safari hii inakuwa ni nafasi ya familia yao pia kuungana nao kutembelea nchi hiyo kwa mara yao ya kwanza.

Kundi hilo lina jumla ya zaidi ya albamu 15 ambazo zinazidi kuwaweka katika nafasi nzuri huku wakipata mialiko ya kutumbuiza katika nchi mbalimbali duniani.