Jumamosi , 8th Nov , 2014

Msanii mwenye historia nzito katika game ya muziki Bongo, Mr Nice amesema kuwa, kwa sasa lengo lake kubwa katika muziki ni kusaka pesa na Heshima pekee, na umaarufu si kitu tena kwake kwasababu alikwishaupata katika kiwango cha kupitiliza.

Mr Nice

Mr Nice ambaye yupo katika mchakato wa kuachia rekodi mpya maalum kwa kuwaheshimu wanawake, amesema kuwa licha ya mtazamo wa tofauti ambao watu wanao juu yake, bado anashikilia rekodi ya kuwa msanii anayefanya show nyingi nnje ya nchi, akiwa anatarajia pia kuwa msanii wa kwanza wa Bongo Flava kwenda kufanya show katika bara la Australia.