Mrembo aliyezaa na Barakah afunguka mazito

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Mzazi mwenza wa msanii Barakah The Prince, Caren Simba amesema aliamua kuachana na msanii huyo wakati ana ujauzito wake baada ya kuona ameanzisha mahusiano mengine na Najdattan.

Kushoto ni Caren Simba, kulia ni Barakah The Prince na Najdattan

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Caren Simba amesema yeye ndio alikuwa wa kwanza kuwa na Barakah The Prince ila alikuwa hataki kujulikana.

"Mimi na Barakah tumekuwa kwa muda mrefu ila aliyekuwa anajulikana ni Naj, wakati yeye yupo na Naj mimi nilikuwa na ujauzito wake na tukaachana kwa sababu ya huyo Naj, sikuwa mchepuko bali ni mwanamke wake kabisa, hatukuwa tayari kuweka mahusiano yetu wazi hivyo Naj ndio akatumia hiyo nafasi" amesema Caren Simba 

Caren Simba amesema kwa sasa yeye na Barakah The Prince wana uhusiano wa kawaida kama mzazi mwenzie pia anamsaidia kutoa ushirikiano kwenye upande wa malezi ya mtoto wao.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.