Jumatatu , 26th Jul , 2021

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja wasanii wa kike wa Bongo Fleva  Nandy, Hamisa Mobetto na Zuchu wamekamata nafasi za juu kwenye Trending on Music huko YouTube.

Picha ya Wasanii Nandy, Mobetto na Zuchu

Wasanii hao wamefanikiwa kupenya mbele ya majina makubwa kama Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize ambao hata kwenye 5 bora hawamo hii ikiwa ni rekodi ya kipekee kwani mara kadhaa ilizoeleka wasanii hao kutawala karibu maeneo mengi yanayohusu sanaa.

Nandy anashika namba 1 kupitia wimbo wake “Nimekuzoea” akifuatiwa na Mobetto na remix ya “Ex wangu” huku Zuchu akishika namba 3 kupitia “Nyumba Ndogo” huku nyimbo zote hizo zikiwa zina zaidi ya views Milioni 2.