Jumatatu , 25th Jul , 2016

Baada ya Mr. T Touch kuachana na studio ya Free Nation iliyokuwa chini ya Nay wa Mitego nakuenda kufungua studio yake bila ya kufahamika sababu hasa iliyopelekea kutofautiana kwao,

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nay wa Mitego

ENewz ilimtafuta Nay wa Mitego pamoja na Mr. T Touch waweze kutudadavulia kisa na mkasa kamili.

Nay wa Mitego alipoulizwa kuhusiana na sababu ya wawili hao kuachana alifunguka kwakuweka wazi kuwa show aliyo andaa Touch mkoani Songea inaweza ikawa sababu kubwa kwakuwa yeye alishindwa kuhudhuria “Mpaka sasa sijajua sababu iliyopelekea yeye kuondoka japo moja ya sababu ni pale niliposhindwa kufika katika show aliyoandaa mkoani Songea na nilimuahidi kumpa alichotaka na kumuomba Radhi pia kama nisingeweza kufika”.

Pamoja na hayo Enewz ilitaka kufanhamu mbali na kutengena huko je wapo tayari kufanya kazi pamoja na Mr. T Touch ambapo Nay wa Mitego alisema kuwa akihitaji mikono ya T alisema hana tatizo Mr. T Touch hivyo ikitokea anawimbo unahitaji uwepo wake hatosita kumfata.

Hata hivyo Mr. T Touch alpo ulizwa kuhusiana na kama ni kweli Nay kutofika kwenye show ndio sababu ya kutengena au la, Yeye alisema “Pamoja na kuwa Nay hakufikia katika show niliyoandaa lakini hiyo sio sababu ambao ingeweza kusababisa sisi tutengane lakini kuna issue tu ambazo zipo nyuma yetu ambazo nisingeweza kuziweka wazi kwa kipindi hiki ila kwa sasa watu wajue kwamba sipo tena chini ya free nation”.

Lakini alipo ulizwa kuhusu kufanya tena kazi na Nay wa Mitegoa, T alikuwa na haya ya kusema “Kwa sasa Nay akija kwenye studio yangu atalipia kama wanamuziki wengine tofauti na awali nilikuwa nikimfanyia kazi bure”.