Jumatatu , 12th Oct , 2015

Baada ya kun'gara kwa muigizaji nyota aliyetwaa tuzo ya Oscar Lupita Nyongo, hivi sasa nyota inazidi kung'ara katika familia yao ambapo kaka yake na Lupita anayeitwa Peter amekula shavu kuigiza huko Hollywood nchini Marekani.

muigizaji nyota wa nchini Kenya Lupita Nyongo akiwa na kaka yake Peter Nyongo

Peter Nyongo (21) anatarajia kuigiza katika filamu yake ya kwanza kabisa iliyobatizwa jina Nocturnal Animals ambayo ni moja ya simulizi maarufu ya kitabu kilichotungwa mwaka 1993 na mwandishi Austin Wright.

Bado haijajulikana ni uhusika upi ambao Peter atakaoucheza katika filamu hiyo inayotarajiwa kuwa tayari hapo mwakani, ambapo itawahusisha waigizaji mbalimbali wa kimataifa wakiwemo Amy Adamsa, Jake Gyllenhaal, Kim Basinger na wengineo wengi.