Jumanne , 15th Sep , 2015

Mkali wa michano Ney wa Mitego amewasisitiza wasanii wa tasnia mbalimbali za burudani nchini kutowekeana chuki au kuweka kipaumbele sana katika pesa wakati huu wa kampeni mbalimbali za wagombea wa vyama vya siasa.

Mkali wa michano Ney wa Mitego

Ney ameongea na enewz akisema kuwa wasanii ni vioo vya jamii na wanatakiwa kuweka umoja na si kutengana sababu tu ya kutofautiana itikadi kupitia vyama vyao ambavyo vinachuana katika kumtafuta kiongozi bora atakayeleta mabadiliko ndani ya nchi.