Jumanne , 17th Mar , 2015

Ikiwa imepita miezi isiyopungua mitano baada ya msanii Ney wa Mitego kumpata mwanae wa tatu anayefahamika kwa jina Munis, staa huyo ametoa kauli nzito kuwa kwa sasa hana mahusiano wala mapenzi yoyote kwa mama wa watoto wake.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Ney wa Mitego

Kauli hiyo iliyoonekana kuwashangaza mashabiki wa msanii ambapo Ney pia amesema kuwa mapenzi yake yote kwa sasa yapo kwa wanawe tu.

Ney ambaye kwa sasa pia kuna tetesi za kuwa anatarajia mtoto mwingine, tetesi ambazo amezikanusha kiutata, amesema kuwa kwa sasa ahitaji kabisa mwanamke, na watoto wake pekee ndio wanampa nguvu na kumhamasisha kujituma kila siku, na hapa anaeleza zaidi.