Alhamisi , 17th Dec , 2015

Mwigizaji maarufu wa Nollywood, Osita Iheme amekamilisha ujenzi wa mradi wake wa mamilioni ya Naira, Hoteli ya kifahari ambayo ameipatia jina The Resident ambayo aliweka wazi juu ya ujenzi wake mwezi Agosti mwaka huu.

Mwigizaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, Osita Iheme

Nyota huyo ambaye amejijengea jina kubwa kutoka filamu ya Aki na Ukwa, amefanya sherehe kubwa kuadhimisha hatua kubwa ya kukamilisha ujenzi wa Hoteli hiyo ambayo itaanza kufanya kazi hivi karibuni.

Mbali na ujasiriamali, Osita amemaliza masomo yake ya Mawasiliano ya Umma kutoka chuo kikuu cha Enugu State huko Nigeria.