Ijumaa , 11th Sep , 2015

Msanii wa muziki Peter Okoye kutoka kundi la P Square ameamua kutumia uwezo wake wa kusakata dansi kutengeneza nafasi ya wenye kipaji kama hicho kuonesha uwezo wao kupitia kipindi cha uhalisia kinachofahamika kama Dance with Peters.

staa kutoka kundi la muziki la P Square, Peter Okoye

Star huyo kutokana na uwezo na nafasi yake kubwa, atakuwa ndio muamuzi mkuu wa vipaji hivyo vya wasakata dansi akishirikiana na mwalimu wa dansi maarufu duniani Kaffy Oluwatoyin, akiwa amekwishaendesha usahili Afrika Magharibi, Abuja, Benin, Accra na Lagos.

Wakati hayo yakiendelea huko Nigeria, hapa nyumbani mashindano ya Dance 100 2015 ya kusaka kundi kali la Dance kwa mwaka huu yanaendelea, makundi 10 ya yaliyofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo yakiwa kambini kujifua kuelekea tarehe 19 mwezi huu ambapo watapambania nafasi 5 za fainali.