Ijumaa , 25th Jul , 2014

Rapa Proffesa Jay, ametoa habari kwa mashabiki wake kukaa tayari kwa jiwe jingine jipya linalokwenda kwa jina Tatu Chafu, ambayo ameweka wazi kuwa video yake ni kutoka kwa muongozaji mkali kabisa anayefahamika kwa jina la Hefemi.

msanii wa muziki nchini Proffesa Jay

Kuhusiana na kazi hii, Jay amesema itashirikisha wakali, Hussle J pamoja na Nigger Jay, moja likiwa jina aliloanza nalo safari ya muziki, mpaka kubadilika kuwa Nigger Jay na sasa Professa Jay.

Kazi hii inatarajiwa kuleta pamoja ladha zote za Jay kutoka kipindi alipoanza muziki ikiwa imetayarishwa studio za Mwanalizombe, na habari hizi zinakuja wakati mashabiki wakisubiri kazi safi kabisa ya Video ya ngoma ya 'Kipi Sijasikia' ft Diamond Platnumz.

msanii wa muziki, Proffesa Jay, Tanzania