Ijumaa , 25th Dec , 2015

Muigizaji anayezidi kujitengenezea jina kupitia fani ya uigizaji filamu nchini mwanadada Rachel Bithulo, yupo katika mchakato wa kumalizia kuigiza katika filamu mpya iliyobatizwa jina 'Dead Samson'.

Muigizaji wa filamu nchini mwanadada Rachel Bithulo

Rachel ameongea na enewz kuwa hii ni moja kati ya filamu ambayo ameonesha uwezo wake mahiri akikiri kuwa ameweza kuimarika na kuungana na waigizaji nyota nchini wakiwemo Ahmed Makambaza, Albert Thadei na wakali wengine kama Awadhi na Sogadi.

Rachel aongea na enewz kuhusiana na filamu hiyo mpya ya 'Dead Samson' inayotarajiwa kuwafikia mashabiki na wadau wa filamu kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, huku akiwa tayari ameigiza filamu maarufu kama 'Kidudu Mtu', 'Claritha', 'Why Me', na nyinginezo nyingi.