Jumapili , 17th Jan , 2016

Muigizaji wa filamu nchini almarufu kama Rachel ambaye amefanya vyema katika filamu ya 'Dead Samson' ametoa ya moyoni kuhusiana na fani yake ya uigizaji baada ya kuwa msanii wa muziki.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Rachel

Rachel ameiambia enewz kuwa alijitahidi sana kuingia katika sanaa ya muziki lakini aligundua kuwa ni kupoteza tu muda kutokana na ukweli kuwa amejikita katika uigizaji wa filamu tu.

Aidha ametoa pongezi kubwa kwa diva anayeshika chati ndani na nje ya nchi mwanadada Vanessa Mdee kwa kuweza kuitangaza vyema nchi kupitia juhudi zake katika muziki.