Alhamisi , 10th Dec , 2015

Msanii wa muziki Mowzey Radio amezungumzia tetesi za kutengana na mama mtoto wake msanii wa muziki Lilian Mbambazi na kueleza kuwa licha ya maneno mengi ya wenye chuki, mwanamke huyo bado ni mke wake na ataendelea kuwa mkewe milele.

Msanii wa muziki nchini Uganda Moze Radio na mama mtoto wake Lilian Mbabazi wakiwa na mtoto wao

Maneno hayo ya Radio yanakuja kufuatia taaarifa za uzushi kuwa, yeye na Lilian wameshindwa kuendelea kutokana na tabia ya kuchepuka iliyopitiliza ya msanii huyo.

Radio ameongeza kuwa, yupo tayari kupambana na yeyote ambaye atakuwa kikwazo katika mapenzi yake na Lilian, maneno aliyoyatoa jukwaani wakati akitumbuiza, kuonesha kuwa ameumizwa kwa kiasi kikubwa.