Jumatano , 25th Mar , 2015

Mwigizaji mahiri kutoka nchini Nigeria, Ramsey Noah Jnr ameeleza sababu ya kupotea kwake kwa muda katika filamu mbalimbali za Nollywood, sababu yake ikiwa ni kulenga ujio mpya katika tasnia hiyo akizingatia bajeti ya kutosha na ubora wa kazi.

muigizaji nyota wa nchini Nigeria Ramsey Noah

Noah amesema kuwa, kwa sasa anajiepusha na kazi rahisi za filamu ambazo mtazamaji anaweza kuona mwisho wake toka mwanzo, na kusema kuwa kazi anazolenga sasa zinahitaji muda, kwa kuwa zinahitaji wawekezaji watakao-eleweshwa na kuelewa namna watakavyohusika na kufaidika katika filamu hizo.

Kufuatia kauli hiyo kutoka kwa Ramsey Noah Jnr, mwenye uwezo na uzoefu mkubwa katika tasnia ya uigizaji, mitaa inasubiri kwa hamu kuona project yake mpya itatengewa bajeti ya kiasi gani na vilevile utofauti wake kiujumla.