Alhamisi , 19th Mar , 2015

Star wa muziki Linex Sunday, amezungumzia mapokezi ya ngoma na video ya Salima aliyomshirikisha Diamond Platnumz, ikiwa ina wiki sasa toka kuachiwa kwake.

Wasanii wa bongofleva Linex na Diamond Platnumz

Mkali huyo amesema video hiyo imekuwa ikitoboa sehemu mbalimbali peke yake kutokana na kisa chake kuwa ndiyo uhalisia wa watu wengi.

Linex amesema kuwa, mbali na watazamaji wengi wa kazi hiyo katika mtandao, ameweza kupata pia mahojiano na vituo mbalimbali kutoka nje ya Tanzania, kitu ambacho kimemshangaza na kumpa moyo pia, ikiwa ni ishara pia ya muziki wa Tanzania kuendelea kuvuka mipaka.