Ijumaa , 14th Aug , 2015

Joto la shangwe za tukio kubwa kabisa la kihistoria katika sekta ya burudani hapa Bongo la Party in The Park, linazidi kupanda baada ya ujio wa kishindo wa moja ya kundi litakalofanya onyesho siku ya kesho la Sauti Sol kutoka Kenya kutua Bongo.

wasanii wa muziki wa kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya wakiwa wamewasili leo asubuhi uwanja wa ndege wa JK Nyerere

Kutoka Uwanja wa JKNyerere Jijini Dar es Salaam, eNewz tukiwa sehemu ya mashuhuda tumekutana na kundi hilo lenye mafanikio makubwa kabisa kitaifa na kimataifa, na hivi ndivyo walivyesema kuhusiana na shughuli ya kesho Party in The Park.

Jioni ya leo pia watatua Mafikizolo, Beatenberg, Xoli, Qness na Blackmotion kumbuka tu, onyesho litafanyika kesho pale The Green Oysterbay Kenyatta Drive Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 1 Jioni .