Jumatatu , 8th Dec , 2014

Siku ya tatu na ya mwisho ya maonyesho makubwa ya mavazi, Swahili Fashion Week 2014 imeweka historia nyingine katika ulimwengu wa mitindo kwa wabunifu mitindo mahiri kuonyesha ubunifu wa hali ya juu katika collection za mavazi yao mwaka huu.

maonyesho ya mavazi na mitindo swahili fashion week 2014

Swahili Fashion Week imeenda sambamba na ugawaji wa tuzo kwa wadau mbali mbali waliofanya vizuri katika vipengele tofauti vya tuzo za maonyesho hayo.

Katika onyesho hili kubwa lililoshereheshwa na mtayarishaji mahiri wa vipindi kutoka EATV, Bhoke Egina, wabunifu wenye uwezo wa aina yake Martin Kadinda, Manju Msita, Innocent Dorkenoo, Gabriel Mollel, Ann Nisa Abayas na Palse South Afrika waliweza kuonyesha mitindo ya mavazi yao ambayo iliyoweza kuvutia umati wapenzi wa mitindo kwa kiasi kikubwa.