Ijumaa , 2nd Jan , 2015

Mwanadada Sola Ogudugu ambaye ndiye mama wa mtoto wa staa wa muziki Wizkid wa huko nchini Nigeria, ameonekana akiwa na ukaribu wenye utata na mwanaume mwingine, ambaye ni mtoto wa mwanaharakati Femi Falana anayeitwa Folarin a.k.a Falz huko Nigeria.

Mwanadada Sola Ogudugu wa Wizkid akiwa na Folarin a.k.a Falz kutoka nchini Nigeria

Hatua hii ya Sola, imeonekana kuchochewa na kitendo cha baba mtoto wake star wa muziki Wizkid, kuonesha dhahiri kumtenga na kutoka na wasichana wengine huku muziki ukiendelea kutengeneza daraja kubwa kabisa kati yao.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Wizkid na timu yake kufuatia hatua hii ya Sola kuonesha kuwa hisia za kimapenzi kati ya wawili hawa zimekwishakufa siku nyingi licha ya kuendelea kuunganishwa na mtoto waliyenaye.