Jumamosi , 27th Jun , 2015

Solo Thang, staa wa muziki ambaye kwa sasa anaendesha shughuli zake huko Dublin Ireland, anajinoa kwa rekodi mpya baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, sambamba na hili akijiweka sawa kufungua kampuni na kuendeleza NGO yake kupitia project ya S.U.M.U.

Solo Thang katika jukumu la malezi ya mwanae

Solo Thang ameahidi pia kujiweka sawa kimuziki baada ya kumaliza kabisa masomo, akiwa anaonesha kimatendo harakati za project hiyo ya SUMU ikimaanisha Sitaki Ujinga Maradhi na Umasikini, itakayoanza kuzaa matunda katika jamii ya kitanzania katika siku za mbeleni.