Jumanne , 29th Dec , 2015

Wakiwa wanaadhimisha miaka 20 ya kusheherekea umoja wao wa kudumu katika kundi, wanamuziki maarufu wa kundi la Spice Girls la nchini Uingereza wanatarajia kuungana tena kwa ujio mpya hapo mwakani.

Kundi maarufu la miondoko ya Pop, Spice Girls

Kundi hilo linalowaunganisha Mel B, Emma Bunton, Geri Halliwell, Victoria Beckham na Mel C, wanaungana tena kwa ajili ya maandalizi makubwa kwa ajili ya kusheherekea ujio wao mpya hapo mwakani.

Imepita takribani miaka mitano tokea habari za kurudi upya kwa kundi hilo maarufu ambapo bado haijawekwa wazi ni ujio utakaokuwa na muendelezo au ni kwa ajili tu ya kusherehekea miaka 20 ya kundi lao.