Alhamisi , 19th Nov , 2015

Ujio wa nyota wa filamu wa kimataifa, Angelina Jolie nchini Kenya, huenda ukawa umekaribia tayari kabisa kwa kufanya kazi ya kuongoza filamu ya 'Africa' itakayohusu maisha ya mdau mkubwa wa uhifadhi wa maliasili, Richard Leakey.

nyota wa filamu wa kimataifa, Angelina Jolie

Ugeni huu mzito wa Angelina huko Kenya umethibitika baada ya taarifa kuwa yeye ndiye atakayekuwa muongozaji wa filamu yenyewe ambayo picha zake zitapigwa huko Kenya, kwa mujibu wa maelezo ya Richard Leakey mwenyewe ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 70.

Filamu hiyo pia itakuwa na mchango mkubwa katika kampeni za kupambana na majangili na kurejesha kasi ya utalii ambayo ilitikiswa na mashambulizi ya kigaidi kwa muda.