Jumatatu , 25th Oct , 2021

Msanii na Mfanyabiashara kutoka Marekani, Kanye West ametambulisha mwonekano wa toleo jipya la viatu vyake “YZY NSLTD BT” rangi ya "Khaki" ambavyo vitaingia sokoni mwezi Novemba mwaka huu.

Picha ya YEEZY INSULATED BOOT

Muundo wa YEEZY INSULATED BOOT ni kama mguu wa Tembo ambapo vilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika onyesho la “YEEZY Season 8 runway” mwezi Machi 2020 na vitauzwa kwa dola 250 zaidi ya Ths. laki 576.