Alhamisi , 24th Apr , 2014

Waajiri nchini Tanzania wametakiwa kutoa maelekezo sahihi kwa wafanyakazi wao juu ya matumizi ya Kemikali katika sehemu ya kazi sambamba na miongozo muhimu ili kuwalinda dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza katika sehemu za kazi.

Kemikali

Wito huo umetolewa leo jijini Dar-es-salaam na Mkuu wa shirika la Maendeleo nchini National Development Co operation (NDC) Bw. Gideon Nassari wakati wa mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi salama ya kemikali katika sehemu za kazi.

Gedion ametoa wito huo katika mkutano uliwakutamnisha mashirika, taasisi na makampuni mbalimbali ya-kiserikali na yasiyo ya-kiserikali.

Nassari amesema Takwimu zinazonesha kwamba karibu watu 375,000 wanakufa kila mwaka duniani kote kutokana na madhara yatokanayo na kemikali sehemu za kazi huku watu milioni 86 wanapata ulemavu wa aina mbali mbali.