Jumanne , 4th Mar , 2014

Wakili wa Utetezi wa mwanaridha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo ameanza kumhoji jirani wa mteja wake aliyeiambia mahakama jana kuwa alisikia mwanamke akipiga mayowe na kuomba msaada siku ya tukio la mauaji Februari 14, 2013.

Katika kesi hiyo Pistorius anadaiwa kumuua rafiki wake wa kike mwanamitindo na muigizaji wa kwenye runinga, Reeva Steenkamp, kosa ambalo amekanusha.

Pistorius alimuua kwa kumpiga risasi Reeva kwa madaia kuwa alidhani kuwa ni mtu aliyemvamia nyumbani kwake katika siku hiyo ambayo hutambulika kama Siku ya Wapendanao Duniani.