Ijumaa , 5th Jun , 2015

Hatimaye star wa muziki wa nchini Kenya, WANGECHI ameachia video ya ngoma inayobeba hisia na pia hadithi ya wakati mgumu aliyopitia kutoka kunusurika kifo katika ajali mbaya kabisa iliyopoteza maisha ya rafiki yake wa karibu mwishoni mwa mwaka jana.

Wangechi

Video ya kazi hiyo ni kazi ambayo imefanywa na Moses Osidiana kutoka Brain Works ikiwa ni ujio na ladha tofauti kabisa ambao tayari wadau wameona umemrudisha msanii huyu katika nafasi nzuri ya juu kwa upande wa sanaa yake.

Video hiyo inayokwenda kwa jina Cardiac Arrest, imeachiwa ikiwa ni takriban wiki tatu baada ya kutoka rekodi yenyewe ambayo imeweza kugusa hisia za wengi kutokana na kile anachokiimba.