Jumatatu , 23rd Mar , 2015

Mpambano mkali wa masumbwi unatarajiwa kufanyika Jijini Dar katika ukumbi wa Diamond Jubilee Ijumaa hii tarehe 27, na kutoa nafasi kwa watu wote kushuhudia mapambano makali kabisa kuwahi kutokea ya ndondi, sambamba na burudani ya muziki.

muigizaji wa filamu nchini Tanzania Irene Uwoya

Tukio hili la aina yake litahusisha mapambano jukwaani ya mabondia Karama Nyilawila na Thomas Mashali, Japhet Kaseba na Mada Maugo, Ashraf Suleiman na Joseph Rabotte toka USA na vile vile Pambano kubwa kabisa Machi 27 watakutana Mohamed Matumla na Wang Xin Hua toka China ambaye ametua nchini leo.

Wasanii kutoka tasnia za sanaa na muziki wameendelea kuonesha msisimko mkubwa kuelekea tukio hili kubwa kama wanavyozungumza nasi hapa.

Hii haijawahi kutokea popote pale, wote tunakutana Diamond Jubilee Machi 27 kuanzia saa moja kamili jioni, na endelea kutegea sikio EA Radio vilevile EATV kujua namna unavyoweza kujishindia tiketi kushuhudia mpambano huo wa The Night of Knockout #NiNgumiTu.