Jumanne , 9th Dec , 2014

Wakati Tanzania Bara ikiadhimisha miaka 53 ya Uhuru wake, mbali na shughuli mbali mbali za kitaifa zilizofanyika kuadhimisha siku hii kubwa kihistoria, wasanii mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kuonesha uzalendo wao.

Muigizaji wa bongo movie Elizabeth Michael aka Lulu

Wasanii hao kwa pamoja wameonesha uzalendo wao kwa kuizungumzia siku hii na kuonesha mapenzi yao kwa nchi yao Tanzania kwa namna tofauti.

Kati ya wasanii ambao wameifungukia siku hii ni pamoja na Bob Junior ambaye ameitakia heri Tanzania bara kwa siku yake ya kuzaliwa nchi hii, pia msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, vilevile Ali Kiba kati ya wengine wengi waliotoa pongezi zao.

eNewz tunaungana na watanzania wote kuitakia Tanzania Bara maadhimisho mema ya miaka 53 tangu kupata Uhuru wake wakati huo ikijulikana kama Tanganyika. HAPPY INDEPENDENCE DAY.