Jumatano , 9th Jul , 2014

Msanii nyota wa nchini Nigeria Wizkid anayetarajia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa manamo tarehe 16 mwezi Julai mwaka huu amepanga kufanya kitu kikubwa na cha kukumbukwa katika siku hiyo muhimu.

Msanii Wizkid wa Nigeria

Wizkid atakayetimiza miaka 24 amepanga kusheherekea birthday yake kwa kuwaalika marafiki zake katika bonge moja la pati ambalo litafanyika katika meli binafsi huko Miami nchini Marekani.

Tukio hilo kubwa limepangwa kufanyika baada ya nyota huyo atakapotumbuiza katika tamasha kubwa la muziki liliobatizwa Live Nation Concert litakalofanyika Jijini New York.